TUNGO KIRAI

Tungo kirai:
Tungo kirai ni kikundi cha maneno chenye kutoa taarifa fulani lakini hakina muundo wa kiima na kiarifu. Katika sehemu hii miundo ya tungo huhusisha maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalum unaozingatia uhusiano uliopo baina ya neno kuu na maneno mengine.
Aina za tungo kirai:        
Kirai nomino (KN):
Kirai nomino ni aina ya tungo kirai ambayo hutawaliwa na nomino au uhusiano na nomino na neno au mafungu ya maneno mengine.
Virai nomino huundwa kwa vipashio mbalimbali. Vipashio hivyo ni kama ifuatavyo:-
A.    Nomino peke yake ( N )
Mfano;
Ø  Baba analima.

Ø  Mwalimu alikimbia.

B.     Nomino mbili au zaidi (N + N ).
Mfano;
Ø  Asha na Fatma wanacheza.
              
Ø  Nyota na mwezi vinang’aa.

C.     Nomino na kivumishi (N + V ).
Mfano;
Ø  Mbuzi watano wamekufa.
              
Ø  Mtoto mzuri ameanguka.
    
D.    Kiwakilishi peke yake. (W)
Mfano;
Ø  Sisi tunasoma SUZA.

Ø  Watano watakuja kesho.
    
E.     Kiwakilishi na kivumishi ( W + V ).
Mfano;
Ø  Mzuri yule amepona.
           
Ø  Wachafu watano watazomewa.
                  
F.      Nomino na kishazi tegemezi.
Mfano;
Ø  Mzee uliyemuona jana ni bibi yangu.

Ø  Mtoto aliyezaliwa leo ni mlemavu.

Kirai Kitenzi (KT):
Kirai kitenzi ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika uhusiano wa kitenzina neno au na mafungu mengine ya maneno. Neno kuu katika kirai kitenzi huwa ni kitenzi. Kirai kitenzi kimejigawa katika vipashio vifuatavyo:-
       I.            Kitenzi peke yake ( T ).
Mfano;
Ø  Anaruka.
Ø  Anacheza.
Ø  Anaimba.
    II.            Kitenzi kisaidizi kimoja au zaidi ya kimoja na kitenzi kikuu (Ts + Ts + T ).
Mfano;
Ø  Alikuwa anacheza.
                   
Ø  Alikuwa anataka kupika.
                              
 III.            Kitenzi, nomino na kielezi. ( T + N + E).
Mfano;
Ø  Anakula ndizi harakaharaka.
                         
Ø  Tulipika chai jikoni.
                       
 IV.            Kitenzi kishirikishi na shamirisho ( t + Sh )
Mfano;
Ø  Ni mzuri.
      
Ø  Si mwalimu.
           
Kirai kielezi (KE):
Kirai kielezi ni nini?
Kirai kielezi ni kirai ambacho hueleza kuhusu namna utendaji wa jambo ulivyo. Mfano inaeleza namna tendo linavyotendeka, wakati linapotendeka na mahali linapotendeka.
Mfano;
v  Amepigwa sasa hivi.
v  Huimba mara kwa mara.
Pia kirai kielezi kinaweza kuwa na kielezi zaidi ya kimoja.
Mfano;
v  Amekula haraka mno.
v  Nitawahi mapema asubuhi.
Kirai kivumishi (KV):
Kirai kivumishi ni nini?
Kirai kivumishi ni aina ya kirai ambacho huivumisha nomino au kiwakilishi. Virai vivumishi vimeundwa na vipashio mbalimbali. Vipashio hivyo ni kama ifuatavyo:-
1)      Kivumishi ns kielezi (V + E)
Mfano;
v  Fupi hasa.
v  nene kweli.
2)      Kivumishi na kirai nomino ( V + KN )
Mfano;
v  -enye duka kubwa.
v  enye pesa nyingi.
3)      Kivumishi na kirai kitenzi (V + KT ).
Mfano;
v  -enye kuumwa mguu.
v  -enye kupika wali.
4)      Kivumishi na kirai kiunganishi (V + KU )
Mfano;
v  -zuri wa kutamanika.
v  -tovu wa nidhamu.
Kirai kiunganishi (KU):
Kirai kiunganishi ni nini?
Kirai kiunganishi ni kirai ambacho huunganisha huunganisha maneno tofauti au vikundi vya maneno.
Mfano;
v  Katika safari.
v  Kwa huruma yako

1 comment:

<marquee>YALIYOMO</marquee>

MAANA YA TUNGO AINA ZA TUNGO TUNGO NENO TUNGO KIRAI TUNGO KISHAZI SENTENSI