Sentensi:
Senensi ni nini?
Sentensi ni kifungu cha
maneno chenye kiima na kiarifu ambacho huleta maana iliyokamili. Kwa kawaida
sentensi huwa na miundo mikuu miwili. Miundo hiyo ni:-
v Kiima.
v Kiarifu.
Kiima:
Kiima ni sehemu ya
sentensi ambayo hukaliwa na mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezwa. Katika
sentensi, kiima kutokea kyshoto mwa kitenzi. Mfano;
Ø Mama
anapika.
Ø Embe zimeharibika.
Vipashio vya kiima:
ü Nomino
peke yake. Mfano;
Mtoto
anacheza.
ü Nomino
na kivumishi. Mfano;
Watoto
wote ni watundu.
ü Nomino
na Nomino. Mfano;
Baba
na mama wanakima.
ü Kivumishi
na Kiwakilishi. Mfano;
Vile
vyao viliokotwa kuke.
Kiarifu:
Kiarifu ni sehemu ya
sentensi ambayo hukaliwa na kitenzi ambacho huarifu tendo lilivofanywa,
linavyofanywa au liutakavyofanywa. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika
sentensi kwani huweza husimama bila kiima. Mfano;
Juma anacheza mpira.
Watoto wanaimba vizuri.
Vipashio vya kiarifu:
ü Kitenzi
kikuu peke yake. Mfano;
Anasoma gazeti.
Anakwenda sokoni.
ü Kitenzi
kisaidizi na kitenzi kikuu. Mfano;
Wahida alikuwa anasomesha.
Walimu walikuwa na kikao.
Aina za sentensi:
Kuna aina kuu nne (4)
za sentensi. Nazo ni;
ü Sentensi sahili:
Ni aina ya sentensi ambayo hujengwa na kishazi huru kimoja. Mfano;
Ali
analima shamba
ü Sentensi changamano:
Ni aina ya sentensi ambayo hujengwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi
tegemezi kimoja au zaidi. Mfano;
Nyumbu aliyepigwa risasi amekimbia.
Mbwa aliyepata kichaa muogope.
ü Sentensi ambatano:
Ni aina ya sentensi ambayo huundwa na sentensi mbili au zaidi. Mfamo;
Mama anapika na baba anafua.
Magazeti huuzwa na watu hununua.
ü Sentensi shurutia:
Ni aina ya sentensi ambayo ina vishazi tegemezi viwiwli au zaidi ambavyo
utegemezi wake hutokana na mofimu –nge, -ngali, -ngeli, ki n.k. zinazojitokeza
katika kitenzi. Mfano;
Angelijibu maswali yote, angelifaulu
mitihani yake.
Akija tutaondoka.
Akinipa nitampenda.
No comments:
Post a Comment