TUNGO KISHAZI



  • Kishazi:

Kishazi ni nini?

Kishazi ni aina ya tungo chenye kitenzi ambacho huweza kujitosheleza au kutojitosheleza. Yaani kuweza kuleta maana inayotarajiwa au hakiwezi kusimama peke yake kikaweza kuleta maana kamili inayotarajiwa. Mfano;

v  Mzee analima.

v  Mtoto aliyekuja jana…

Katika mifano hiyo tunakuwa kwamba, tungo ya kwanza imeweza kujitosheleza kimaana lakini katika tungo ya pili haikuweza kujitosheleza kimaana kwani haikuweza kuekeza huyo mtoto aliyekuja jana amefanya kitu gani.

Sifa za kishazi:

ü  Kishazi ni lazima kiwe kitenzi.

ü  Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea hata kama sentensi ikiondolewa katika muktadha wa sentensi kuu.

ü  Vishazi vingi hasa vishanzi huru huwa na kiima dhahiri.

ü  Vishazi, hasa vishazi huru kwa kawaida huwa na kitenzi kimoja kikuu.

Aina za vishazi:

Kuna aina kuu mbili za vishzi. Navyo ni:-

a.       Vishazi huru.

b.      Vishazi tegemezi.

Vishazi huru:

Vishazi huru ni vishazi ambavyo hujitosheleza kimaana na kuwa na vitenzi vikuu. Yaani vishazi huru huweza kusimama peke yake na kutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo. Mfano;

Ø  Mzee aliyekuja ameshaondoka.

Ø  Gari tulilokuja nalo limeondika.

Sifa za vishazi huru:

Ø  Kishazi huru huwa na hadhi ya sentensi sahili

Ø  Havina urejeshi.

Ø  Hujitosheleza katika kuleta maana ya tungo.

Ø  Huwa na vitenzi vikuu.

Vishazi tegemezi:

Vishazi tegemezi ni aina ya vishazi ambavyo huwa na kitenzi kisaidizi ambacho hakikamilishi ujumbe. Kwa kawaida vishazi tegemezi hutegemea vishazi huru ili kuweza kukamilisha maana halisi ya ujumbe uliokusudiw

a. Mfano;

v  Mbuzi aliyeumia mguu…

v  Maji yaliyomwagika…

v  Watoto waliopotea…

Sifa za vishazi tegemezi:

ü  Hutawaliwa na urejeshi.

ü  Huweza kuondoshwa katika sentensi bila kuharibu maana kamili ya sentensi mzima.

ü  Huweza kutangukiwa au kufuatwa na vishazi huru.

No comments:

Post a Comment

<marquee>YALIYOMO</marquee>

MAANA YA TUNGO AINA ZA TUNGO TUNGO NENO TUNGO KIRAI TUNGO KISHAZI SENTENSI